ZINAZOVUMA:

Ikulu ya Dodoma kuzinduliwa rasmi Mei 20

Ikulu ya Chamwino Dodoma inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Mei 20 na...

Share na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Raisi imesema kuwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Ikulu mpya ya Chamwino Mei 20 mwaka huu.

Watumishi mbalimbali wa serikali wanatarajiwa kuhamia Ikulu hiyo mpya wakiongoza na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassani.

Ujenzi wa Ikulu hiyo ambayo kwa muonekano wa jengo kwa nje ni sawa na ule wa Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam umetekelezwa na wakandarasi wazawa na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Mei, 2020 Hayati Rais John Magufuli akiwa na Marais Wastaafu waliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ikulu hiyo ambayo ilikuwa ni ndoto ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere.

Oktoba 10, 1973 Mwalimu Nyerere alitangaza uamuzi wa kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma lakini pamoja na kujengwa kwa makazi ya Rais Serikali ilikuwa bado haijahamia Dodoma.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya