ZINAZOVUMA:

Ibrahim Raisi kuweka sheria kali za makosa ya hijab

Rais Ibrahim Raisi wa Iran aemsema kuwa ukaguzi wa makosa...

Share na:

Rais wa Iran Ebrahim Raisi anataka kuweka sheria kali kwa wanawake kwa makosa ya hijab (hijabu) licha ya maandamano makali nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Ujerumani DPA siku ya Jumapili (Aprili 21), Raisi alisema kuwa kuheshimu vazi la Hijabu sio tu ni jambo la kidini bali pia ni wajibu wa kisiasa na kisheria kwa wanawake wa Iran.

Rais aliongeza kuwa hakuna shaka yoyote kwamba ukaguzi lazima uendelee kutekelezwa mara kwa mara.

Matamshi ya rais huyo yamejiri mwezi mmoja baada ya polisi na walezi wa maadili nchini Iran kwa mara nyingine tena kuzidisha msako mkali dhidi ya ukiukaji wa hijabu.

Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha mapigano kati ya wanawake na walinzi wa maadili wakati wa ukaguzi.

Kifo cha mwanamke wa Kikurdi nchini humo Mahsa Amini akiwa chini ya ulinzi wa polisi mnamo Septemba 2022 kilisababisha maandamano nchini kote dhidi ya utawala wa Kiislamu na kanuni zake za mavazi.

Amini alizuiliwa na polisi wa maadili kwa sababu ya hijabu inayodaiwa kutokwenda vizuri.

Siku chache baadaye, alifariki katika kituo cha polisi, ikidaiwa kuwa ni matokeo ya vurugu za polisi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya