ZINAZOVUMA:

Hali ya Nigeria yamchanganya Raisi Tinubu

Raisi wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza hatua za kukabiliana na...

Share na:

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza hatua kadhaa za kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha, ikiwemo kutoa tani laki mbili za nafaka ya akiba ili kupunguza gharama za maisha nchini humo.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Mei, Rais Bola Tinubu amechukua maamuzi kadhaa yanayokusudia kuimarisha uwekezaji wa muda mrefu, lakini hatua hizo zimeathiri vibaya uchumi wa raia wa Nigeria na kuongeza umaskini katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Mwezi uliopita, Rais huyo aliondoa ruzuku ya mafuta, na kusababisha bei ya petroli kuongezeka maradufu na kupanda kwa bei ya chakula.

Rais Tinubu amesema hali ya maisha imepanda nchini humo na itawaathiri wananchi wote lakini wanapaswa kutuliaa na kumuamini wakati akipambana ili kurudisha uchumi wa Nigeria.

Aidha katika kile alichokiita kuwapunguzia mzigo wananchi, ameahidi dola milioni 264 kwenda katika kilimo, dola milioni 165 kwenda katika sekta ya biashara za viwango vya kati na ndogo, na dola milioni 99 katika sekta ya viwanda viwanda.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya