ZINAZOVUMA:

Hairuhusiwi kusuka Zanzibar, faini milioni moja

Baraza la Sanaa, Sensa ya filamu na Utamaduni Zanzibar limetoa...

Share na:

Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar limekanusha kuhusu kutoa kibali kwa wanaotaka kusuka kuwa ni shilingi milioni moja.

Na pia limetoa ufafanuzi kuwa mwanaume yeyote haruhusuwi kusuka Zanzibar na atakayekamatwa akiwa amesuka adhabu yake ni kulipa faini ya shilingi milioni 1 au kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja.

Akizungumza Katibu Mtendaji baraza hilo, Dkt. Omar Adam amesema kwa mujibu wa utaratibu wa mila na desturi za Zanzibar mtoto wa kiume haruhusiwi kusuka nywele za aina yoyote, na sheria inakataza mtu yeyote kukiuka mila na desturi zilizopo.

Kuhusu watalii wanaofika visiwani humo ikiwa watawajibika na utaratibu wa ulipaji faini, amesema faini hiyo inawahusu watu wote walio ndani na wageni kutoka nje ya Zanzibar.

“Duniani hakuna mipaka ya sheria, Uchina ukikamatwa na unga maana yake hukumu yako ni kifo, haijalishi umetoka wapi, kwa hiyo na hii ni sheria ipo Zanzibar kwa watu wote waliokuwepo kwenye mipaka ya Zanzibar.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya