ZINAZOVUMA:

Fifa yamfungulia kesi Rais wa soka Hispania

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limemfungulia kesi Rais...

Share na:

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limefungua kesi za kinidhamu dhidi ya Rais wa shirikisho la soka la nchini Hispania Luis Rubiales kwa tabia yake alioionesha kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Rubiales alimbusu mshambuliaji Jenni Hermoso kwenye midomo baada ya Hispania kushinda dhidi ya Uingereza na kufanikiwa kuwa mabingwa wa kombe hilo.

Hata hivyo taarifa kutoka nchini Hispania zinasema Rubiales anatarajiwa kutangaza kujiuzulu na tayari amewataarifu watu wake wa karibu kuhusu uamuzi huo.

Rubiales alikuwa amepoteza uungwaji mkono na wachezaji, serikali, FIFA, na hata mashirika ya ndani ambayo yanategemea bajeti ya shirikisho la mpira duniani.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,