ZINAZOVUMA:

Fataki na baruti marufuku kesho kwa Mkapa

Kamanda kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema...

Share na:

Kuelekea mchezo wa kesho Mei 28, 2023 wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger ya Algeria itakayopigwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar saa 10:00 jioni, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema tayari limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu maeneo yote ya kuzunguka uwanja ndani, nje na barabarani.

“Hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo,” amesema

Amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki au baruti uwanjani, kurusha chupa au kitu chochote.

Ameeleza kuwa hayo ni baadhi ya makosa ya mambo ya kiusalama kwenye viwanja vya soka.

“Jeshi la Polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo zimepigwa marufuku na vyama vya soka FIFA, CAF na TFF. Watakao kaidi, watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Jeshi la Polisi linawatakia mashabiki wa soka kushangilia kistaarabu,”amesema.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya