ZINAZOVUMA:

EWURA imesema kuwa Tanzania ina mafuta ya kutosha

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA...

Share na:

Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (EWURA) imetoa onyo kwa kampuni zinazohodhi mafuta na kuzitaka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni zinazosimamia biashara ya mafuta ya petroli nchini na masharti ya leseni zao za biashara.

Onyo hilo limetolewa na EWURA Jana Jumatatu Julai 17,2023 na kueleza kuwa wamepokea taarifa ya uwepo wa baadhi ya kampuni za mafuta kuhodhi mafuta kwa masrahi binafasi.

Aidha tarifa hiyo imeeleza kuwa zipo kampuni za mafuta zinasemekana kupakia mafuta kutoka kwenye maghala pasipo kuyauza na nyingine kukataa kuuza mafuta kwa wamiliki wa vituo wasio kuwa na ubia au mikataba nao.

“Ewura inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa nchi ina mafuta ya kutosha katika maghala ya kuhifadhia mafuta na meli zenye shehena ya mafuta kutoka nje ya nchi zinaendelea kuingia na kushusha mafuta kama kawaida chini ya uratibu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA),” imesema Ewura Katika taarifa yake ya jana Julai 17, 2023.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya