ZINAZOVUMA:

EU yaingilia mzozo Niger

Umoja wa Ulaya umekosoa kinachoendelea Niger na kuamua kuiunga mkono...

Share na:

Umoja wa Ulaya umekosoa kile kinachoendelea Niger na kutaka Rais Mohamed Bazoum aachiwe mara moja baada ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi.

Kwa mujibu wa mkuu wa sera za Mambo ya Nje katika umoja huo, Josep Borrell, kuna wasiwasi mkubwa kutokana na hali inayoendelea hivi sasa ya kushikiliwa kwa Rais Bazoum na familia yake.

EU inasema taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa Mohamed Bazoum na familia yake, wamenyimwa chakula, umeme na huduma za matibabu kwa siku kadhaa.

Haya yanajiri wakati huo Marekani nayo imesema kwamba itawaajibisha wanajeshi waliochukua madaraka nchini humo kuhusu usalama wa Rais Mohamed Bazoum, familia yake pamoja na maofisa wote wa serikali wanaozuiliwa.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken pia ameeleza nchi yake inaunga mkono juhudi ya Jumuiya ya ECOWAS kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya