Tume ya Uchaguzi ya Ethiopia (NEBE) imetangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kuwa ni Juni 1, 2026. Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Ethiopia, Melatwork Hailu ameviambia vyombo vya habari nchini humo kwamba shughuli ya kuanzisha ofisi za matawi na kuhakikisha vituo vya kupigia kura vinafaa kwa kupigia kura imeshafanyika.
Ameongeza kuwa vyama vya siasa vimepewa mafunzo ili kutangaza ratiba zao kwa umma. Kuandaa uchaguzi nchini Ethiopia kunakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto za kiusalama kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyohusisha Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray na vikosi vya serikali kuanzia mwaka 2020 hadi 2022 katika eneo la Tigray.



