ZINAZOVUMA:

Ethiopia yarejesha matumizi ya mitandao

Ethiopia imeruhusu matumizi ya mitandao ya kijamii baada ya kuifugia...

Share na:

Mamlaka nchini Ethiopia zimerejesha matumizi ya mitandao ya kijamii baada ya kuifungia kwa miezi mitano.

Mamlaka hizo zimerejesha huduma za kimtandao baada ya kufungia Mitandao ya Facebook, Telegram, TikTok na YouTube tokea Februari 9, 2023 kufuatia mvutano kati ya Serikali na Kanisa la Orthodox.

Kwa Miezi 5 wale tu waliokuwa wanatumia programu ya mtandao wa kibinafsi (VPN) ndio walioweza kuingia kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, hivyo kuzidisha matumizi ya vifurushi ya Internet.

Kulingana na Jumuiya ya Mtandao, kukosekana kwa huduma za Mtandao kumegharimu Ethiopia Dola Milioni 42 za Marekani, sawa na takribani Tsh. Bilioni 102.6 kwa sababu ya athari za biashara.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya