ZINAZOVUMA:

Erdogan: Nafaka za “Black Sea” zinazihitajika

Raisi Erdogan anaendeleza mazungumzo ya nafaka za Black Sea, Hajakata...
Erdogan akihutubia
Erdogan akihutubia

Share na:

Mwezi julai, Urusi ilijitoa katika mpango wa kuuza nafaka uliosukwa na Uturuki pamoja na Umoja wa Mataifa.

Mpango huo uliazimia kuruhusu nafaka kutoka Urusi na Ukraine kwenda katika mataifa wahitaji bila kuathiriwa na vita.

Hata hivyo, urusi ilisema inajitoa kwa sababu mbalimbali ikiwemo, ya nafaka ikichukuliwa zaidi kutoka Ukraine na sio Urusi.

Baada ya mzozano mkubwa katika mpango huo, baadae Urusi iliweka vizuizi vya nafaka kutoka Ukraine.

Huku akisema sababu ni za kiusalama zaidi kwa Urusi, ikiwemo kukuta viashiria vya vilipuzi katika meli ya nafaka.

Mbali na kuweka vizuizi, Urusi pia ililipua bandari ya Odessa nchini Ukraine, hali iliyosababisha kupungua kwa nafaka kutoka nchi hizo mbili.

Hata hivyo Raisi wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, Amekusudia kuhuisha mpango huo wa nafaka kutoka Urusi.

Na katika kusisitiza hilo, baada ya kikao cha mataifa ya G20, Rais Erdogan alisema kuwa Mpango wowote wa nafaka wa Bahari Nyeusi (Black Sea), usipomuhusisha Urusi hautadumu.

Na kuongeza kuwa Urusi, Ukraine na Uturuki zitaendeleza maongezi yao juu ya mpango huo wa nafaka za Black sea.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,