Raisi wa Uturuki Recep Erdogan anaunga mkono mpango wa Ukraine kujiunga na umoja wa nchi za Ulaya NATO na kuweka wazi mbele ya Raisi wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskiy kuwa Ukraine wanastahili kuwepo katika umoja huo.
Raisi Erdogan ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Raisi Zelenskiy.
Aidha Raisi Erdogan amesema anataka amani ipatikane kati ya Urusi na Ukraine ikiwa tayari imetimia siku 500 tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
“Mazungumzo ya amani hayatamfanya yoyote kuwa mjinga” amesema Raisi Erdogan.
Zelenskiy ameshukuru Erdogan kwa kumuunga mkono ambapo imeonekana kuwa ni ishara njema kuelekea katika mkutano mkuu wa NATO unatarajiwa kuanza siku ya jumanne katika Mji wa Vilnius, Lithuania.