ZINAZOVUMA:

ECOWAS yaiwekea vikwazo Niger

Jumuiya ya umoja wa nchi za Magharibi ECOWAS umelipa wiki...

Share na:

Umoja wa nchi za ECOWAS umelitaka jeshi la nchini Niger kumrudisha madarakani Rais Mohammed Bazoum vinginevyo utachukua hatua kurejesha utaratibu wa Kikatiba.

Viongozi wa umoja huo wa Afrika walikaa kikao cha dharula na kuamua kuupa wiki moja utawala wa kijeshi nchini Niger kuachia madaraka.

Hilo lisipofanyika basi jeshi la Niger litalazimika kukabiliana na matumizi ya nguvu na kuwekewa vikwazo vya kifedha.

Aidha aliyekuwa mlinzi Mkuu wa Rais Bazoum, General Abdourahmane Tchani ndio alitangazwa kama kiongozi Mkuu wa nchi hiyo baada ya kufanyika mapinduzi.

Nchi za Afrika ya Magharibi imekua ikakabiliwa na mapinduzi ya kijeshi mara kwa mara.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya