ZINAZOVUMA:

EAC yamtaka Raisi Tshisekedi kuonesha heshima

Umoja wa nchi za Afrika Mashariki umemtaka Raisi wa jamuhuri...

Share na:

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imemtaka kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu hatua ya mataifa ya kikanda ya kupeleka vikosi katika jaribio la kuleta utulivu katika maeneo ya mashariki mwa nchi yake.

Hatua hiyo imefuata baada ya Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi kulishutumu jeshi la Afrika Mashariki kwa kutofanya kazi yake, akionya huenda likaombwa kuondoka nchini humo kufikia Juni.

Pia Raisi huyo alishutumu jeshi hilo kwa kushirikiana na waasi wa M23.

Aidha kwa upande wa nchi mwanachama, Katibu Mkuu wa EAC Peter Mathuki asema hajapokea mawasiliano yoyote kuhusiana na malalamiko ya Raisi Tshisekedi, akisema masuala yoyote yatakayoibuliwa yatajadiliwa na wakuu wa nchi za EAC.

“Naomba tuheshimu na kuamini wanachama wa mkutano wa EAC kwa sababu najua wana nia ya kutatua suala hili,” Bw Mathuki alisema.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya