Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa mwandishi wa jarida, E. Jean Carroll katika duka moja mjini New York miaka ya 1990.
Jopo la majaji tisa lilifikia uamuzi huo baada ya mashauriano ya chini ya saa tatu siku ya Jumanne ambapo pia imemkuta na hatia ya kumkashifu mwandishi huyo kwa kuita madai yake ni ya uongo.
Mahakama iligundua kuwa Carroll (79) alikuwa amethibitisha vya kutosha kwa mahakama kwamba Trump alimnyanyasa kingono karibu miaka 30 iliyopita katika chumba cha kubadilishia nguo.
Mahakama ya Manhattan imemuamuru Trump amlipe mwandishi huyo takriban dola milioni tano kama fidia.
Hata hivyo wakili wa Donald Trump amesema kwamba mteja wake huyo atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.