ZINAZOVUMA:

Dkt Ndumbaro aikaribisha Al Ahly kufungua ‘Academy’ Tanzania

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro ameikaribisha...

Share na:

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameikaribisha Klabu ya AL Ahly ya nchini Misri ije kuwekeza katika Sekta ya michezo nchini Tanzania kwa kufungua ‘Academy’ ya michezo ili kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamichezo.

Dkt. Ndumbaro ameikaribisha Klabu hiyo namba moja Afrika hivi karibuni alipofanya ziara kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na timu hiyo katika Jiji la Cairo, nchini Misri.

Timu hiyo pia inamiliki kituo cha Gezira Center ambacho kinaendesha viwanja vya michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa wavu, mpira wa netiboli, gofu na riadha.

AL Ahly ni miongoni mwa Klabu kubwa Afrika iliyoanzishwa mwaka 1907 ikiwa na wanachama zaidi ya 200,000 na mashabiki zaidi ya milioni 1 nchini Misri.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya