ZINAZOVUMA:

Charles Hilary atoa ufafanuzi Bagamoyo kumilikiwa na Zanzibar

Msemaji Mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ametoa ufafanuzi kwanini...

Share na:

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary amefafanua suala la eneo lililopo Makurunge Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesema eneo hilo linaitwa Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) na lipo kwenye mipango ya Uwekezaji wa Zanzibar.

Charles Hilary amefafanua jinsi eneo hilo lilivyoingia kwenye miliki ya Zanzibar, amesema,

“Marehemu Rais Julius Nyerere alilikabidhi kwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe, lilikuwa likitumika kuwanenepesha ng’ombe kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.

“Kulikuwa na Meli inaitwa Jitihada iliyotumika kuwasafirisha ng’ombe, baadaye mradi huo ulififia na hakukuwa na ng’ombe wanaosafirishwa, eneo likabaki tu kwa muda mrefu.

“Watu wengi wameona liko tupu wakanza kuvamia, kuna watu walianza kuuziwa na wengine wakawa wanaambiwa jenga haraka” Amesema.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya