ZINAZOVUMA:

Cameroon: Waasi wateka wanawake 30

Waasi nchini Cameroon wameteka wanawake zaidi ya 30 huku wakiwajeruhi...

Share na:

Wapiganaji wanaotaka kujitenga katika eneo la kaskazini magharibi lenye machafuko nchini Cameroon, wamewateka nyara zaidi ya wanawake 30 na kujeruhi wengine wengi.

Wanawake hao walitekwa nyara katika kijiji cha Big Babanki, karibu na mpaka na Nigeria, kwa madai ya kupinga amri ya kutotoka nje na kutozwa kodi na watu hao wanaotaka kujitenga.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Cameron vinaripoti kuwa idadi ya wanawake waliopotea imeonekana kuwa ni kubwa zaidi hadi ya wanawake 50.

Aidha Maafisa wa Cameron walisema baadhi ya wanawake waliteswa vikali na waasi hao waliojihami na silaha ambao mara kwa mara huwateka nyara raia kwa ajili ya fidia.

Kiongozi wa waasi hao Capo Daniel aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba wanawake hao wanaadhibiwa kwa kuruhusu kudanganywa na serikali ya Cameroon.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,