ZINAZOVUMA:

Brice Nguema Raisi wa mpito Gabon

Wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Gabon wamemchagua jenerali Brice Nguema kuwa...

Share na:

Maofisa wa jeshi nchini Gabon ambao jana Jumatano Agosti 30, 2023 walihusika kumpindua Rais Ali Bongo, wamemteua mwanajeshi mwenzao, Jenerali Brice Nguema kuwa Rais wa mpito wa Taifa hilo.

Wakati Nguema anateuliwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Rais wake aliyepinduliwa bado anashikiliwa na wanajeshi hao katika makazi yake huku familia yake ikitenganishwa naye.

Baada ya kutangazwa kuongoza nchi hiyo, Jenerali Nguema alizunguka mitaani nchini humo akiwa amebebwa juu na wanajeshi wenzake huku wakimshangilia.

Gabon imekuwa chini ya utawala wa familia ya Bongo kwa zaidi ya miaka 50 ambapo Ali Bongo alikuwa Rais akimfuatia Baba yake mzazi, Omar Bongo ambaye alifariki mwaka 2009.

Uamuzi wa Jenerali Nguema kuongoza nchi hiyo maarufu kwa uzalishaji wa mafuta ulifanywa baada ya wanajeshi hao kupiga kura.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya