Msomaji Bingwa wa Quran duniani kutoka Misri, Sheikh Mahmood Shahat Anwar, ambae pia ni mtoto wa aliekua msomaji wa Quran Bingwa wa Zamani Marehemu Qari Sheikh Shahat, anatarajiwa kuingia Tanzania leo Jumanne Agosti 29 2023.
Sheikh Shahat anatarajiwa kuingia nchini Tanzania saa sita mchana katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere Dar Es salaam na kupokelewa na umma wa kiislamu.
Ujio wa Sheikh Shehat nchini Tanzania umeratibiwa na taasisi ya ‘Khidma Tul Quran’ chini ya Mkurugenzi wake Sheikh Ali Mohammed Saleh.
Msomaji huyo wa Quran atafanya ziara katika misikiti mbalimbali ikiwepo msikiti wa Mtoro Kariakoo ambapo ndipo atakapoanzia siku ya kesho Jumatano baada ya swala ya Magharibi.