ZINAZOVUMA:

Benki ya dunia imemteua Raisi mpya

Benki ya dunia imemteua Ajay Banga mwenye asili ya kihindi...

Share na:

BODI ya wakurugenzi watendaji wa benki ya dunia (WB) imemteua Ajay Banga kuwa raisi wa benki hiyo kwa muhula wa miaka mitano kuanzia Juni 2, 2023.

Banga ataongoza mchakato wa mageuzi ya kundi la Benki ya Dunia, kama ilivyojadiliwa katika mikutano ya majira ya masika ya Aprili 2023, na juu ya matamanio na juhudi zinazolenga kukabiliana na changamoto ngumu zaidi za maendeleo zinazokabili nchi zinazoendelea.

Taarifa ya WB imesema wakurugenzi watendaji walifuata mchakato wa uteuzi uliokubaliwa na wanahisa mwaka 2011. Mchakato huo unajumuisha uteuzi wa wazi, unaozingatia sifa na uwazi ambapo mwanachama yeyote wa benki anaweza kupendekezwa na Mkurugenzi Mtendaji au Gavana kupitia Mkurugenzi Mtendaji. Hii ilifuatiwa na uchunguzi wa kina na mahojiano ya kina ya Bw. Banga na Wakurugenzi Watendaji.

Banga mwenye asili ya India amepongezwa na Raisi wa marekani Joe Biden kwa uteuzi huo akichukua nafasi ya David Malpas ambae alikosolewa kwa msimamo wake juu mabadiliko ya tabia ya nchi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya