Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeridhishwa na kasi ya ukuaji uchumi nchini unaotarajiwa kukua kwa asilimia 5.2 mwaka huu.
Taarifa ya BoT imeeleza kuwa mwendendo wa ukuaji wa uchumi nchini umeendelea kuwa wa kuridhisha kutokana na kuimarika kwa mazingira ya kibiashara, uwekezaji unaoendelea kufanywa na sekta ya umma na binafsi, kuimarika kwa shughuli za utalii na ongezeko la ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi.
BoT ilieleza kuwa Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) imeridhishwa na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kupunguza ongezeko la ukwasi kwenye uchumi ili kudhibiti mfumuko wa bei wakati ikichangia ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta ya fedha.
Utekelezaji huo uliwezesha ongezeko la ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, na kusaidia kuweka mazingira mazuri ya kuendelea kuimarika kwa shughuli za kiuchumi nchini.