ZINAZOVUMA:

Bei ya petrol yazidi kupanda Zanzibar

Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji Zanzibar...

Share na:

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza ongezeko la bei ya mafuta ya petroli kwa asilimia 10 visiwani Zanzibar kutoka Sh 2,700 kwa lita mwezi uliopita hadi Sh 2,970 mwezi huu ikiwa ni ongezeko la Sh 270.

Taarifa iliyotolewa jana na mamlaka hiyo ilisema bei hizo mpya zitaanza kutumika leo Agosti 9,2023 ambapo bei ya mafuta ya dizeli imepanda kwa asilimia nne kutoka Sh 2,746 kwa lita moja hadi Sh 2,843 ikiwa ni ongezeko la Sh 97.

Aidha, taarifa hiyo imeonesha kuwa mwezi huu hakutakuwa na ongezeko la bei kwa mafuta ya taa ambapo bei yake itabaki ile ile ya mwezi uliopita ya Sh 2,921 kwa lita moja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,mafuta ya ndege yamepanda kwa asilimia nane kutoka Sh 2,190 kwa lita mwezi uliopita hadi Sh 2,365 mwezi huu ambapo kuna ongezeko la Sh 175.

Sababu ya mabadiliko hayo imeelezwa kuwa ni nikuongezeka kwa bei ya mafuta katikasoko la dunia na dola ya Marekani.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya