ZINAZOVUMA:

Bei ya Mafuta Kenya yazidi kupanda kama Tanzania

Bei ya mafuta nchini Kenya imepanda tena Kwa mara nyingne...

Share na:

Bei ya mafuta nchini Kenya inaendelea kuongezeka, hii ni kulingana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) ambayo imefanya marekebisho ya bei za mafuta ambazo zitaanza kutumika Septemba 15.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka EPRA, bei mpya za mafuta jijini Nairobi zitakuwa kama ifuatavyo: Petroli itauzwa kwa KSh 211.64 kwa lita, dizeli kwa KSh 200.9 na mafuta ya taa kwa KSh 202.61.

Kulingana na EPRA, bei mpya za petroli zimeongezeka kwa KSh 16.96 kwa lita, dizeli imeongezeka kwa KSh 21.32 kwa lita, na mafuta ya taa yameongezeka kwa KSh 33.13 kwa lita, ikilinganishwa na bei za awali.

EPRA pia imebainisha kuwa bei hizi zinajumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani ya asilimia 16 (VAT) kulingana na kifungu cha Sheria ya Fedha ya 2023.

Wakati huo katika jiji la Dar es salaam, Tanzania mafuta yamepanda mpaka kufikia TSh3,213 kwa lita moja ya petroli na TSh3,259 kwa lita moja ya dizeli.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya