Polisi nchini Uingereza wamekamata mimea ya bangi yenye thamani ya hadi £130m na kuwakamata zaidi ya watu 1,000 katika msako mkubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo dhidi ya uhalifu wa kupangwa.
Zaidi ya mimea 180,000 iligunduliwa katika uvamizi uliofanyika kote Uingereza na Wales katika msako huo.
Maafisa wa polisi pia walikamata bunduki 20, pesa taslimu £636,000 na kilo 20 za kokeini, zenye thamani ya ya £1m.
Operesheni hiyo imeelezewa kuwa ni muhimu zaidi na ya aina yake kuwahi kutekelezwa na vyombo vya sheria vya Uingereza.
Operesheni hii iliyalenga magenge ya uhalifu ambao pia wanahusika katika makosa mengine kama vile utakatishaji fedha, ulanguzi wa dawa za kulevya na vurugu.