Brumelda Zuma, Mtoto wa Jacob Zuma Rais wa Zamani wa Afrika Kusini na kiongozi wa chama cha MK, ameapishwa baada ya kuteuliwa kuwa mbunge wa chama hicho.
Brumelda ameapishwa wiki chache baada ya mtoto mwingine wa Zuma, kujiuzulu ubunge kwa tuhuma za kupeleka watu 17 kupigana kwa ajili ya Urusi.
Binti huyo wa Zuma ameapishwa yeye na wabunge wengine watatu wa chama chake cha uMkhonto weSizwe.
Sakata hili la binti mmoja kujiuzulu ubunge, na mwingine kuteuliwa na limegubikwa na ushawishi wa familia ya Zuma, na kuonyesha azma ya zuma kuhakikisha lazima mwanae awepo katika bunge.
Bado polisi inaendelea na uchunguzi juu ya sakata hilo, kwani ni kosa kisheria kwa raia wa Afrika kusini kupigana vita kwa niaba ya nchi nyingine, bila ridhaa ya serikali.
Na binti aliyemshitaki Duduzile aitwaye Nkosazana, amesema kuwa ndugu zake nane wapo katika kundi hilo la vijana 17 waliorubuniwa.
Huku Duduzile akitaja sababu ya kujiuzulu kuwa, aweze kupata muda na nafasi ya kuwatafuta vijana hao 17, kwani yeye alidhani wanaenda kwa ajili ya mafunzo na si kupigana vita.



