Mahakama nchini Thailand imeagiza kusimamishwa Ubunge kwa muda kwa Pita Limjaoroenrant ambae pia ni mgombea wa kiti cha uwaziri Mkuu nchini humo baada ya kukutwa na kesi ya kujibu.
Kwa mujibu wa mahakama Pita hakustahili kugombea katika uchaguzi uliofanyika Mei 14 kutokana na umiliki wake wa vyombo vya habari nchini humo.
Maamuzi ya mahakama yaliyotolewa leo jumatano yamemkuta Pita na hatia ya kuwa na hisa katika chombo kimoja cha habari nchini humo ambapo kwa mujibu wa sheria ya Thailand hairuhusiwi kwa mgombea kuwa na hisa au mmiliki wa chombo cha habari.
Pita ambae ametia nia ya kugombea uwaziri Mkuu nchini humo amesema kuwa hisa alizonazo katika chombo hicho cha habari ni mali alizorithi kutoka kwa Baba yake na sio zake.