Jake Lang na Wamarekani wenzake wanaopinga Uislamu waliandamana nje ya moja ya jumuiya kubwa za Kiislamu na misikiti huko Texas.
Jake alileta nguruwe wadogo watano kama sehemu ya maandamano yake dhidi ya Uislamu wa Marekani nje ya Kituo cha Kiislamu cha Plano Mashariki.
Tukio lililovuta hisia kali kutoka kwa wanajamii wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.
Hakuna vurugu zilizotokea mbali na kuwa Umati huo ulisheheni watu wa pande zote mbili Waislamu, na wapinga uislamu baada ya polisi na vikosi vya usalama vya binafsi kulinda usalama eneo hilo.
kwa watu wote waliohudhuria eneo hilo bila vurugu licha ya ujumbe wa chuki uliokuwa ukitolewa na Lang wakati wa tukio.
Maandamano haya yaliratibiwa nje ya Msikiti wa East Plano Islamic Center (EPIC) mjini Texas huku Jake Lang akisimama kwenye kitanda cha lori akiendelea kupinga Uislamu.
na wakati wa hotuba yake ya chuki alikuwa akishika kichwa cha nguruwe huku Qur an ikiwa imewekwa kwenye mdomo wa kichwa hicho cha nguruwe kama dihaka kwa Uislamu.
Viongozi wa Dini na makundi ya haki za binadamu wamelaani kitendo hicho na kukisema kama cha kichochezi na uvunjifu wa amani na mshikamano kwenye jamii kwa ujumla.
Waumini wa kiislamu kutoka katika jumuiya hiyo ya EPIC waliokusanyika eneo hilo, walionekana wakigawa chakula kwa watu na waandamani hao wanaopinga uislamu bila kujali ujumbe wao.



