ZINAZOVUMA:

Atumikia miaka 33 gerezani bila hatia

Aliyetumikia zaidi ya theluthi mbili ya kifungo cha miaka 45...
This undated photo, provided the by Los Angeles District Attorney's Office, shows Daniel Saldana, right, flanked by his lawyer Mike Romano, center, and fellow exoneree Frankie Carrillo, back left. Saldana, who spent 33 years in California prison for attempted murder, has been declared innocent and freed. (Los Angeles County District Attorney's Office via AP) Daniel Saldana

Share na:

Mwanaume mmoja huko California nchini Marekani ambaye alikaa gerezani kwa miaka 33 kwa jaribio la kuua ametangazwa kuwa hana hatia na kuachiliwa huru baada ya kubainika kuwa hakuwepo eneo la tukio.

Daniel Saldana, ambaye sasa ana umri wa miaka 55, alipatikana na hatia ya kufyatulia risasi gari akitoka katika mchezo wa soka wa shule ya sekondari huko Baldwin Park, mashariki mwa Los Angeles mnamo 1990.

Kulikuwa na vijana sita ndani ya gari na wawili kati yao walijeruhiwa lakini walinusurika.

Saldana, ambaye alikuwa na umri wa miaka 22 wakati wa shambulio hilo alikuwa akifanya kazi kwa muda za ujenzi. Alikuwa mmoja wa watu watatu walioshitakiwa kwa shambulio hilo na alipatikana na hatia ya makosa sita ya jaribio la kuua na shitaka moja la kufyatulia risasi gari hilo na baadae alihukumiwa kifungo cha miaka 45 jela.

Saldana alionekana na Mwanasheria wa Wilaya George Gascón katika mkutano na waandishi wa habari akitangaza kuachiliwa kwake siku ya Jana Alhamisi, akishukuru kuachiliwa kwake.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya