Dkt Nusrat Praveen wa mfumo wa AYUSH nchini India, aliyepata uteuzi wa serikali ya jimbo la Bihar, amekataa uteuzi huo baada ya kuvuliwa hijabu hadharani katika hafla ya uteuzi Desemba 15 2025.
Daktari huyo alivuliwa hijabu yake na Waziri Mkuu wa jimbo la Bihar, Nitish Kumar hadharani.
Baada ya tukio hilo alipewa ajira ya serikali chini ya kitengo cha AYUSH akitakiwa kuripoti Sabalpur Desemba 20 katika kituo cha afya.
Hata hivyo hakuripoti kazini kama alivyoelekezwa, na familia yake ikasema kuwa fedheha ya kuvuliwa hijabi ilimuumiza kisaikolojia sana na kumlazimu kwenda kuishi na ndugu zake nje ya jimbo hilo.
Aliondoka Bihar na kuelekea kwa ndugu zake hatua iliyochukuliwa kama uamuzi wa heshima binafsi mkubwa na msimamo thabiti wa kimaadili.
Mfumo wa AYUSH unajumuisha Ayurveda Yoga Unani Siddha na Homeopathy ukisimamiwa na wizara ya Afya ya serikali kuu ya India.
Tukio hilo limezidisha mvutano wa kisiasa huku vyama vya upinzani vikimtaka Nitish Kumar ajiuzulu mara moja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Mamlaka za kisheria zimeanza uchunguzi kuhusu mwenendo wake na haki za wanawake, pamoja na heshima ya imani katika umma wa India.



