Serikali ya Afrika Kusini chini ya Raisi Cyril Ramaphosa ipo mbioni kubadilisha sheria ili kukwepa kumkamata Raisi ya Urusi Vladimir Putin.
Uamuzi huo unatarajiwa kufanyika ili kuwa na nguvu ya kuamua mtu wa kumkamata pindi anapotuhumiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Rais wa Urusi,Vladimir Putin ana mwaliko wa kushiriki kikao Agosti 2023 Nchini Afrika Kusini na yupo hatarini kukamatwa kutokana na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine lakini Wenyeji wake hawataki akamatwe kwa kuwa wao hawana upande katika vita hiyo.
Serikali ya Afrika Kusini itawasilisha pendekezo la mabadiliko hayo Bungeni, Juni 2023, wakati upande wa pili Chama cha Upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimesema kitafungua kesi kupinga uamuzi wa Serikali huku wao wakitaka Putin akamatwe akitua Afrika Kusini.