Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, Fikile Mbalula amesema Uchumi wa Nchi hiyo uko kwenye hali mbaya kutokana na kukatika kwa Umeme mara kwa mara
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu huyo ambaye ametaja sababu kuwa ni kukatika kwa Umeme kunakotishia kuzorotesha Ukuaji wa Uchumi.
Mbalula amsema “Kama baadhi masuala hayatopatiwa suluhu, tutakuwa Nchi iliyoshindwa kutokana na Uchumi kuyumba kwa sababu mbalimbali na nyingine zimechangiwa na udhaifu wetu wa kushindwa kusimamia vizuri hali ya Uchumi”.
Kwa mujibu wa Taasisi ya VolunteerInternational, Afrika Kusini inakabiliwa na ongezeko kubwa la Vijana wasio na Ajira wanaofikia 63.4% huku wengi wao wakiishi chini ya Mstari wa Umasikini.