ZINAZOVUMA:

Afrika kusini kumfuata mtuhumiwa wao.

Muhalifu aliyetoroka nchini Afrika kusini amekamatwa Tanzania na anatarajiwa kurudishwa...

Share na:

Wawakilishi wa ngazi za juu wa serikali ya Afrika Kusini watasafiri kuja Tanzania kufuatia kukamatwa kwa mfungwa Thabo Bester aliyetoroka gerezani wakati akitumikia kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini.

Thabo Bester na washirika wake wawili walikamatwa na maafisa usalama wa Tanzania Aprili 8 jijini Arusha kufuatia uwepo kwa hati ya kukamatwa kwake baada ya kutoroka gerezani.

Bester mwenye umri wa miaka 46 alipata umaarufu kufuatia namna alivyokua akiwarubuni wanawake kupitia mtandao wa Facebook ambapo mwaka 2012 mahakama nchini humo ilimtia hatiani kwa kosa la kuwarubuni wanawake wawili huku akiwabaka na kumuua mmoja.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya