Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Abdulrahman Kinana, amesema Raisi Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla inafuatilia kwa ukaribu athari zinazotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
Amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kupeleka fedha za ukarabati wa miundombinu na misaada mbalimbali kuwasaidia watu walioathirika.
Kinana ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wilaya ya Musoma Mjini mkoani Mara, amba owalieleza uharibifu wa baadhi ya miundombinu ya Barabara katika wilaya hiyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
“Serikali inaendelea kufanya tathimini ya uharibifu wa miundombinu ili kutenga fedha za ukarabati maeneo yote ambayo yameathirika”
“Uharibifu wa miundombinu umefanyika katika nchi mbalimbali duniani hata zile zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo na siyo Tanzania peke yake” amesema makamu Mwenyekiti Kinana.