ZINAZOVUMA:

500 hawajulikani walipo mpaka leo kisa kimbunga Freddy

Toka kutokea kwa kimbunga Freddy nchini Malawi hadi hivi sasa...
Men dig in search of survivors and victims in the mud and debris left by Cyclone Freddy in Chilobwe, Blantyre, Malawi, March 13, 2023. REUTERS/Eldson Chagara.

Share na:

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi amesema kimbunga Freddy cha kilichotokea miezi kadhaa iliyopita kimetaabisha nchi yake na kusababisha vifo kwa watu wengi huku wengine wakikosa makazi na kuharibu maisha na miundombinu ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa rekodi rasmi ya serikali idadi ya vifo kutokana na hali hiyo mbaya ya hewa ilikuwa ni zaidi ya watu 507 huku wengine 500 hawajulikani walipo na zaidi ya watu 553,600 wakukosa makazi.

Aidha Rais Chakwera alipongeza juhudi za pamoja za marais wa zamani Bakili Muluzi na Joyce Banda kwa kutafuta fedha za kusaidia kujenga tena makazi kwa raia wao.

Wakati huohuo makundi ya kiraia yamesema Rais ameshindwa kutekeleza ahadi zake na wanamtaka ajiuzulu.

Wanalaumu utawala wake kwa upungufu wa chakula na kushindwa kuboresha hali ya maisha, wameilaumu pia serikali kwa kutumia taasisi za serikali ikiwemo polisi kukandamiza waandamanaji.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,