ZINAZOVUMA:

15 wafa maji kutokana na mvua zinazoendelea

Takriban vifo 15 vimetokea nchini kutokana na mvua zinazoendelea maeneo...

Share na:

Watu 15 wamefariki dunia kutokana na kusombwa na maji ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha nchini katika maeneo mbalimbali.

Takwimu hizo zimetolewa leo April 8 na jeshi la polisi nchini Tanzania

Ambapo jeshi hilo limesema baadhi yao wamefariki dunia wakati wakiwa wanaogelea wengine wakiwa wanavuka katika maeneo ambayo maji yanatirika kwa kasi na wengine ni kutokana na kudumbukia kwenye mashimo na madimbwi yaliyojaa maji

Aidha taarifa imesema miongoni mwa waliofariki ni pamoja na watoto wadogo 12 na watu wazima watatu na kubainisha kuwa vifo hivyo vimetoea ndani ya siku saba pekee

Pia taarifa hiyo imebainisha maeneo ambayo vifo hivyo vimetokea kuwa ni Wilaya ya kalambo Mkoani Rukwa, wilaya ya kilwa mkoani Lindi, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Wialya ya muhenza mkoani Tanga, Wilaya za kibaha na Mkuranga mkoani Pwani, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya na Mkoani Geita

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi nchini limeendelea kutoa wito na tahadhari kwa watu wote hususani wazazi na walezi katika uangalizi wa watoto kwenye msimu huu wa Mvua.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya