Kampuni ya YARA Tanzania imeleta virutubisho vya wanyama, kama bidhaa nyingine katika msururu wa bidhaa zao za kilimo.
Kampuni hiyo ni miongoni mwa kampuni kubwa za pembejeo Tanzania, ni kampuni tanzu ya Yara International na kuna matawi Afrika nzima.
Baada ya kuingiza Mbolea nchini kwa muda mrefu, Yara Tanzania imeona kuna haja ya kungiza virutubisho vya wanyama.
kama ilivyo mbolea za Yara, na virutubisho hivyo pia vinazalishwa na kampuni mama ya Yara International.
Na kampuni hiyo imeona ni bora kuwekeza Tanzania kwa kuingiza virutubisho vya wanyama ili kukuza sekta hiyo nchini.
Mkurugeniz mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Winstone Odhiambo amesema kuwa wataanza kuingiza virutubisho mbalimbali.
“Yara international inatengeneza virutubisho vya wanyama vya hali ya juu, na hivyo tutaanza kuleta kwa mara ya kwanza katika soko la Tanzania” Alisema bw. Odhiambo
Kampuni hiyo inatarajia kuleta virutubisho anuai kwa ajili ya wanyama mbalimbali kwa ajili ya wanyama wote ikiwemo jamii ya kuku.
Huku wakisisitiza kuwa lengo lao ni kuunga mkono juhudi za kuongeza wingi na ubora wa bidhaa zitokanazo na wanyama ikiwemo Nyama na maziwa nchini.
Bw. Odhiambo amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu kwa Afrika, kupata virutubisho hivyo vya wanyama.
Nchi ambazo zimeipiku Tanzania katika kupata virutubisho hivyo ni Afrika Kusini, ikifuatiwa na Kenya.
Kampuni hiyo inatarajia kuzindua rasmi virutubisho hivyo Mkoani Iringa tarehe 19 mwezi Septemba.
Kutakuwa navirutubisho vilivyochanganywa mahsusi kwa ajili ya Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Wanyamapori, Samaki na hata wafugwao kwa kama paka na mbwa.