ZINAZOVUMA:

Yanga sasa kuvuna milioni 20 kila goli

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu...

Share na:

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani ameahidi shilingi milioni 20 kwa kila goli watakalolipata Yanga katika hatua ya fainali na kuahidi kutoa ndege itakayowapeleka Algeria na kuwarudisha Tanzania.

Raisi ameyasema hayo leo tarehe 18/5/2023 wakati wa uzinduzi wa minara ya mfumo wa urushaji wa matangazo ya televisheni ya Azam Media Limited kwa kutumia antenna (DTT)

Yanga atakwenda nchini Algeria katika mchezo wa mkondo wa pili June 3 ambapo atacheza na Usm Alger ikiwa ni fainali ya pili baada ya ile itakayochezwa tarehe 28 Mei kwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Aidha kwa upande mwingine Raisi Samia ameipongeza Azam kwa kuendelea kutoa huduma bora katika vipindi vyao na kukata kiu ya watanzania.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,