Klabu ya Yanga kutoka Tanzania itakutana na klabu ya Usm Alger kutoka Algeria katika hatua ya fainali baada ya siku ya jana kufanikiwa kushinda michezo yao ya nusu fainali.
Yanga alifanikiwa kuifunga klabu ya Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini mabao mawili kwa moja na kufanya magoli ya jumla kuwa nne kwa moja, pamoja na yale Yanga aliyoyapata kwenye mchezo wa awali katika uwanja wa Mkapa.
Usm Alger wamemfunga Asec Mimosas kutoka nchini Ivory coast mabao mawili kwa sifuri na kufanikiwa kuingia fainali huku mchezo wa awali walitoka sare ya bila kufungana.
Fainali za msimu huu za michuano ya CAF zitachezwa mara mbili kwa maana ya nyumbani na ugenini, mechi ya kwanza itakua Mei 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga ataanzia nyumbani na wiki moja baadae itachezwa fainali ya pili nchini Algeria.