ZINAZOVUMA:

Waziri wa Libya afutwa kazi kwa kukutana na Waziri wa Israel

Libya haiitambui Israel na imekua ikiiunga mkono palestina hali iliyopelekea...

Share na:

Waziri Mkuu wa Libya, Abdulhamid Dbeibah ametangaza kumsimamisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Najla al-Mangoush baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen kutangaza kuwa, wawili hao walifanya mazungumzo mjini Rome wiki iliyopita ambayo hayakuwa rasmi.

Wizara ya mambo ya nje ya Libya imeelezea kuwa mkutano huo ulikuwa sio rasmi na kwamba wawili hao walikutana tu bila kupanga, japo taarifa za mkutano huo tayari zimesababisha maandamano katika miji kadhaa ya Libya.

Mzozo huo wa kisiasa ulizuka jana baada ya Wizara ya Mambo ya nje ya Israel kueleza kuwa, mawaziri wa mambo ya nje wa Israel na Libya walikutana wiki iliyopita.

Israel inajaribu kujenga uhusiano wa karibu na nchi nyingi za Kiarabu ambazo zina idadi kubwa ya waislamu kama vile Libya ambayo pia tajiri wa mafuta.

Hata hivyo Libya haiitambui Israel, kwani inaunga mkono hoja ya Palestina, na ndio sababu mkutano huo umezusha maandamano.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya