ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu ataka maamuzi ya mahakama kutekelezwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mamlaka mbalimbali Tanzania kuheshimu maamuzi...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mamlaka mbalimbali nchini kuheshimuwa hukumu halali zitolewazo na mahakamani na iwapo kuna asiyekubaliana na mamuzi hayo, ni vema kukata rufaa na siyo kushindwa kutekeleza.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Mei 11, 2023 bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo ambapo Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani (CCM), ametaka kujua kauli ya serikali kuhusu Mamlaka za Hifadhi kushindwa kurudisha mifugo kwa wafugaji ambao wameshinda kesi.

Mbunge huyo alisema kumekuwa na kilio kikubwa kutoka kwa wafugaji ambao walishinda kesi zao na mahakamani ikaamuru warejeshewe mifugo yao lakini kumekuwa na ukimywa wa muda mrefu kwa mamlaka hizo kutekeleza maagizo hayo halali ya mahakama.

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa ni jambo la kisheria kwamba hakuna anayeweza kupinga amri ya mahakama kwa sababu ni hukumu, basi kama kuna maeneo ambayo yana amri hiyo, basi yatekeleze.

Kauli ya Waziri Mkuu imekuja kukiwa na kelele nyingi kutoka kwa wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa kwenye hifadhi na kupelekwa mahakamani lakini baadhi ya walioshinda kesi hawajarudishiwa mifugo yao.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya