ZINAZOVUMA:

Waziri Kairuki akabidhi magari 43 kwa TARURA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na...

Share na:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amekabidhi magari 43 kwa Watendaji wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Makatibu Tawala Wasaidizi wanaoshughulika na Miuondombinu katika ngazi za Mikoa.

Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 05, 2023 Makao Makuu ya TARURA – Mtumba Dodoma kwa watendaji hao kwa ajili ya kuwawezesha kuboresha utendaji kazi wao.

Waziri Kairuki amesema magari 30 kati ya 43 ni kwa ajili ya matumizi ya Ofisi za Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) makao makuu na mikoa na magari 13 ni kwa ajili ya ofisi za wakuu wa mikoa kwa ajili ya usimamizi wa kazi za miundombinu.

Amesema lengo kuu kukabidhi magari haya kwa TARURA na mikoa ni kuwawezesha kuboresha utendaji kazi, hususan katika utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.”

“Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora kwa wananchi, imeendelea kuwezesha taasisi za umma, hususan Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini, kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari ili kuimarisha utendaji kazi na usimamizi wa miradi”

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya