Mahakama katika mji wa kusini mwa Uganda wa Jinja umewanyima dhamana wanaume sita wanaotuhumiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja ambao wanadaiwa kunaswa kwenye video.
Mwendesha mashtaka alisema washukiwa hao walikuwa sehemu ya mtandao unaowafundisha wavulana wadogo kufanya vitendo hivyo vya ulawiti na kuwaingiza wanaume watu wazima katika mahusiano ya mapenzi yajinsia moja, liliripoti gazeti la Daily Monitor.
Wanaume hao wenye umri wa kati ya miaka 20 na 26 walishtakiwa kwa tabia hiyo iliyo kinyume na maadili.
Mahakama hiyo iliwanyima dhamana washtakiwa kwa misingi kwamba hawatakuwa salama katika jamii.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja tayari ni haramu nchini Uganda lakini bunge limependekeza muswada utakaoleta adhabu kali zaidi ikiwemo adhabu ya kifo.