ZINAZOVUMA:

Waliomtorosha Facebook Rapist waachiwa

Wafanyakazi wa G4S waliosadikiwa kumsaidia muuaji "Facebook Rapist" kutoroka gerezani...

Share na:

Mahakama nchini Afrika Kusini imewaachia huru watu watatu, waliokuwa wakihusishwa na kumsaidia Thabo Bester kutoroka.

Watu hao watatu walikuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S, wakilinda gereza la Mangaung.

Walioachwa huru ni Nastassja Jansen, Thabang Mier and Moeketsi Ramolula, huku wengine lukuki wakibakishwa kwa makosa mbalimbali.

Thabo Bester maarufu kama “Facebook Rapist” ni raia wa Afrika Kusini na mfungwa wa maisha kwa makosa mbalimbali yakiwemo kubaka na kuua.

Mwaka jana alifanikiwa kutoroka katika gereza la Mangaung, kwa msaada wa wafanyakazi mbalimbali wa gereza hilo.

Huku ikisadikiwa kuwa mpango huo ulisukwa Dokta Nandipha Magudumana, ambaye pia inasemekana wana uhusiano na Bester.

Baada ya kutoroka Bester alifanikiwa kutoka nje ya Afrika Kusini, na alikamatwa Arusha nchini Tanzania mwezi Mei 2023.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya