ZINAZOVUMA:

Wajumbe Baraza la wawakilishi lamtaka C.A.G kuomba radhi

Wajumbe Baraza la wawakilishi Zanzibar limemtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa...

Share na:

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameomba mwongozo wakitaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuomba radhi chombo hicho kwa kauli yake aliyoitoa mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwamba kamati zake hazina uwezo wa kufanya kazi.

Kauli hiyo wameitoa Mei 5, 2023 wakati wa kikao cha baraza wakiomba mwongozo wa Spika kuhusu kauli iliyotolewa na CAG, Dk Othman Abbas Ali wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2021/22 Mei 3, 2023 Ikulu Zanzibar.

Wakati akiwasilisha ripoti hiyo CAG alimuomba Rais (Dk Hussein Mwinyi) kuzijengea uwezo kamati za Kudhibiti Hesabu za Serikali (PAC na LAAC) akisema hazina uwezo katika masuala ya Tehama maana kuna vitabu vinne mpaka sasa kamati hizo zimeshindwa kuvifanyia kazi kwa kukosa utaalamu.

Katika kuthibitisha hilo CAG alisema kamati hizo zimeshindwa kufanya uchunguzi wa mifumo ya Tehama ya Sh1.5 bilioni kwa Wizara ya Afya, Sh1.3 bilioni Wizara ya Ujenzi, Sh5 bilioni katika Wizara ya Fedha ambapo zote zinahusu wizi katika mifumo ya Tehama.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya