Uingereza imeona kuuliwa kwa raia wake ni sawa na fadhila za mbuzi kutoka kwa Israel ambayo amekuwa akiikingia kifua. kati ya watu saba waliofariki katika shambulo la msafara wa magari ya World Central Kitchen, watatu ni raia wa uingereza.
Taifa hilo ambalo limekuwa likikingia kifua mashambulizi ya Israel dhidi ya wapalestina wa ukanda wa Gaza, limetaka uchunguzi ufanywe na tume huru ya kmataifa ili kupata uhalisia wa shambulio hilo.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameomba radhi na kusema kuwa mambo kama hayo huwa yanatokea kwenye vita. Hata hivyo bado Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak hajaridhishwa na majibu hayo bali alisisitiza kufanyika uchunguzi ndipo serikali yake itatoa maamuzi.
Majaji wa Uingereza wametoa tamko kali kwa Waziri Mkuu kuwa kuendelea kupeleka silaha kwa Israeli ni kukiuka sheria ya kimataifa. Tamko la serikali ni kwamba linasuburia uchunguzi na kutoa tamko kuhusu kuendelea kuuza silaha au kuacha kuuza silaha kwa Israel. Marekani imewalaumu Israel kwa kutokufanya bidii za kutosha kulinda watu ila hawakutoa kauli yoyote ya kuacha kuisaidia Israel kwenye mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza pamoja na wazayuni kuendelea kuvunja sheria za kivita.
Waingereza waliofariki katika shambulio hilo ni John Chapman (57), James Henderson (33) na James kirby (47), wakiwa wanatokea Dal el Barah kutoa misaada kama wafanyakazi wa shirika la WCK.
Hatma ya ushirikiano kati ya Israeli na Uingereza hasa kwenye kuuziana silaha itategemea zaidi ripoti ya uchunguzi itakapokamilika. Na hili linaweza kusababisha ripoti hiyo ikashushia lawama kundi jingine ili kudumisha uhusiano na chano cha silaha cha Israel.