ZINAZOVUMA:

UN yaitaka Ufaransa kubadili mfumo wa polisi

Umoja wa mataifa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki...

Share na:

Wakati machafuko yaliyotokea nchini Ufaransa kwa wiki nzima yakipungua kasi, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, yameitaka serikali ya nchi hiyo kufanya mageuzi katika vikosi vyake vya polisi na kukabiliana na hatua zenye utata za ubaguzi kwa misingi ya rangi ya ngozi ya mtu.

“Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kurekebisha mfumo wa polisi,” mashirika sita ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na ‘Human Rights Watch’, na “Amnesty International’ yalisema katika taarifa siku yake siku ya jana.

“Huu ndio wakati kwa nchi hiyo kushughulikia kwa umakini masuala ya kina ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi katika utekelezaji wa sheria,” alisema, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu.

Wito huo umekuja baada ya mauaji ya Juni 27, ya kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17, Nahel Mer-zouk, yaliyofanywa na afisa wa polisi nje ya mjiwa Paris.

Tukio hilo lilisababisha maandamano makubwa katika miji takribani 200 nchini Ufaransa katika muda wa wiki moja iliyopita.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya