ZINAZOVUMA:

Ulaya waandamana kupinga mashambulizi ya Gaza

Maelfu ya watu waandamana katika miji mikubwa ya Ulaya kama...

Share na:

Maelfu ya watu katika miji ya London (Uingereza), Madrid (Hispania) na Istanbul (Uturuki) wamejitokeza mitaani kuandamana kupinga vita vya Gaza huku Israel ikiahidi kuendelea na mashambulizi yake huko Rafah, kusini mwa Gaza.

Wakipeperusha bendera ya Palestina na mabango, maelfu wameandamana katika mitaa ya Madrid, nchini Hispania wakitaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza wakisema wanaoumia si askari bali raia.

Umati wa watu ulipenya katika mitaa iliyofungwa katika mji mkuu huo wa Hispania kutoka kituo cha treni cha Atocha hadi eneo la kati la Plaza del Sol, nyuma ya bendera kubwa iliyosomeka: Uhuru kwa Palestina.

Wengi wamebeba mabango yaliyosomeka “Amani kwa Palestina” na “Usipuuze mateso ya Wapalestina”.

Takriban mawaziri sita kutoka baraza la mawaziri la Waziri Mkuu, Pedro Sanchez pia wameshiriki katika maandamano hayo, watano kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha Sumar, pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Oscar Puente wa chama cha Waziri Mkuu cha Socialist Party.

“Tunahitaji kusitishwa kwa mapigano mara moja, kukomesha mauaji na mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia, lazima tufanikishe kuachiliwa huru kwa mateka wote,” Puente amewaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa maandamano hayo.

Katika mji mkuu wa Uingereza, London, takriban watu 250,000 wameshiriki katika maandamano ya kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, kulingana na Kampeni ya Mshikamano wa Palestina (PSC).

Akiripoti kutoka London, mwandishi Harry Fawcett wa Al Jazeera amesema maandamano yanayofanyika London ni kati ya matatu kwa ukubwa tangu kuanza kwa vita huko Gaza mnamo Oktoba.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya