ZINAZOVUMA:

Ulaya Kukumbwa na Joto Kali: Tahadhari ya Hali ya Hewa

Kuanzia wiki ijayo Bara la Ulaya litashuhudia joto kali zaidi...

Share na:

Kuanzia wiki ijayo, baadhi ya maeneo barani Ulaya yanaweza kukumbwa na hali ya joto kali zaidi kuwahi kutokea barani humo.

Hali hii imebainishwa na wataalam wa hali ya hewa, ambapo wametahadharisha kuwa joto hilo linaweza kufikia hadi nyuzi joto 48 jambo linalotishia usalama wa watu, mifugo na mazao.

Mtandao wa Dail Mail umeripoti leo Julai 14, 2023 kuwa upepo mkali wenye joto (Anticlones) umeshuhudiwa ukipuliza kutoka kaskazini mwa jangwa la Sahara kuelekea kusini mwa bara la Ulaya katika siku za hivi karibuni.

Hali hiyo imesababisha kuibuka kwa moto wa porini unaotishia maisha ya watu na wanyama huko nchini Croatia.

Wakati watalii na wenyeji barani humo wakijitahidi kuivumilia hali hiyo, nchi za Hispania, Italia, Ugiriki na Uturuki, joto linatarajiwa kuongeza zaidi ya nyuzi 45 ifikapo mwishoni wa wiki ijayo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya