ZINAZOVUMA:

Uganda: Afungwa miaka 6 jela kwa kumtukana Rais

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa...

Share na:

Mahakama nchini Uganda imemhukumu kijana wa miaka 24 kifungo cha miaka sita jela, kwa kumtusi Rais Museveni na familia kwa njia ya video iliyorushwa kwenye mtandao wa TikTok.

Kijana huyo anayefahamika kwa jina la Edward Awebwa alishtakiwa kwa matamshi ya chuki na kueneza taarifa “za kupotosha na zenye nia mbaya” dhidi ya Rais Yoweri Museveni, Mkewe Bi. Janet Museveni na mwanawe Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mkuu wa majeshi ya Uganda.

Miongoni mwa taarifa za Abebwa zilizofikishwa Mahakama kama za kupotosha, alisema kuwa nchini humo kutwakuwa kutakuwa na ongezeko la ushuru chini ya Rais Museveni.

Pamoja na kwamba alikiri makosa yake na kuomba msamaha, Hakimu Kiongozi wa kesi hiyo alisema kuwa haoneshi kujtia kitendo chake na maneno aliyotumia yalikuwa “machafu sana”.

Katika hukumu ya kesi hiyo Abebwa alihukumiwa miaka 6 jela kama funzo, ili akitoka ajifunze kumuheshimu Rais na Familia yake alisema hakimu Stella Maris Amabilis.

KIjana huyo alihukumiwa kwa mashata manne kila moja miaka 6, na vifungo vyote hivyo vya kesi nne atavitumikia kwa wakati mmoja.

Mashirika ya haki za binadamu yamekashifu mamlaka ya Uganda mara kwa mara, juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa kujieleza kutokana na kesi kama hizi.

Mwandishi wa Uganda aliyeshinda tuzo Kakwenza Rukirabashaija alishtakiwa mwaka 2022, kwa makosa mawili ya “mawasiliano ya kukera” dhidi ya Rais na mwanaye kupitia mtandao wa Twitter.

Pia mwanaharakati na mwandishi Stella Nyanzi ambaye kwa sasa yupo uhamishoni, aliwahi kufungwa baada ya kuchapisha shairi lililomkosoa Rais Museveni.

Kifungu cha “Mawasiliano ya kukera” katika Sheria kimeendelea kutumika mbali na Mahakama ya kikatiba, kuamua kuwa kifungu kipo kinyume na katiba ya Uganda.

MMojwa wa mawakili wa haki za binadamu nchini Uganda Michael Aboneka amesema kuwa Awebwa ameshtakiwa chini ya sheria hiyo ambayo wanaipinga mahakamani kwa sababu “haieleweki”.

Na kuongeza kuwa Rais wa Uganda na familia yake wanapaswa kutarajia kukosolewa “kwa njia yoyote” na “wawe wanasema kwamba watamkamata kila raia wa Uganda kwa kuwakosoa”.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya